2015-02-04

Mbunge wa Kigoma Kaskazini @Zitto Kabwe aliliwa na-------Kilicho Endelea Ni Balaa

Picha:Zitto Kabwe.jpg

HISIA! Mrembo mmoja ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja, ameshindwa kuzuia hisia zake na kuamua kumlilia hadharani Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Zuberi Kabwe.

Tukio hilo lilitokea katika ‘viwanja’ vya Escape One, Jumamosi iliyopita katika maadhimisho ya miaka kumi ya Nyumba ya Vipaji Tanzania (THT).
Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Zuberi Kabwe akiwa na wasanii wa THT jukwaani.


Awali, mrembo huyo huku akiwa na kinywaji chake mkononi, alionekana akielekea jukwaani baada ya kusikia msanii Ali Kiba anapanda stejini kupafomu.

“Weweee huu muda wa maangamizi sasa hivi jembe linakuja stejini ngoja nisogee nikampe kampani Mwana-Dare s salaam nampenda sana jamani Ali Kiba,” alisikika mrembo huyo huku sauti yake ikiashiria alikuwa na kilevi mwilini.


Wakati Kiba akiwa jukwaani, alimuita Zitto jukwaani ndipo mwanadada huyo alipomkimbilia mheshimiwa na kutaka kumkumbatia huku akilia na kusema katika wanasiasa ambao anawakubali, Zitto ni namba moja.

“Zitto… mheshimiwa…mbunge huwa nakukubali sana, dah leo nimepata bahati ya kuonana na wewe nataka tupige picha ya pamoja, mimi sijali watu watanijaji vipi ninachotaka hapa ni picha tu, nyie wapiga picha nipigeni basi maana nikiikosa leo ndiyo basi tena sijui nitamuona wapi,” alisikika dada huyo.

Mwanadada mrembo aking'ang'ania kupiga picha na Mh. Zitto Kabwe.


Kutokana na kuendelea kumg’ang’ania mbunge huyo, watu walibaki midomo wazi na kujiuliza kulikoni lakini bahati nzuri Zitto alifanikiwa kumkwepa mrembo huyo, akapanda jukwaani.

Wakati Zitto akiwa jukwaani na Ali Kiba sambamba na wasanii wengine walioimba wimbo wa Leka Dutigite, mrembo huyo alionekana chini ya jukwaa akitafuta namna ya kugusanisha mkono wake na mwanasiasa huyo kipenzi cha vijana lakini hadi dakika za mwisho, hakufanikiwa!

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...