2015-02-02

Polisi watawanya wananchi kwa mabomu wakidai matuta kwa kufunga barabara

Polisi wakiondoa vizuizi vilivyowekwa na wananchi barabarani. 

Wananchi wakionekana kusikitishwa na kitendo cha polisi kuondoa vizuizi vyao barabarani.Polisi wakiwa wamemweka chini ya ulinzi mmoja wa watu waliokuwa mstari wa mbele kufunga barabara. 

Wananchi wakitawanyika baada ya polisi kupiga mabomu ya machozi. 

WAKAZI wa eneo la Kawe-Bondeni jijini Dar es Salaam jioni hii wameamua kukaa katikati ya barabara eneo hilo wakiishinikiza serikali kuwawekewa matuta wakidai kuchoshwa na ajali za mara kwa mara ambazo zimekuwa zikiondoa uhai wa wapendwa wao wakiwemo wanafunzi. 

Hata hivyo malengo yao hayakuweza kutimia sawasawa baada ya polisi kuingilia kati na kulazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya. 

Wananchi hao wamefikia uamuzi huo baada ya kudaiwa fedha za kulipia gharama za kuhifadhi mwili katika Hospitali ya Taifa Muhimbili. Mwili huo ni wa mwananchi aliyegongwa na gari jana eneo hilo hilo linalolalamikiwa na wakazi hao.

 GPL



0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...