MWANAMUZIKI wa Bendi ya FM Academia, Suzan Chubwa ‘Queen Suzy’ hivi karibuni amejifungua mtoto wa kike na ameeleza kuwa, amefarajika kwani alikaa muda mrefu tangu alipopata wa kwanza wa kiume.
Mtoto wa , Suzan Chubwa ‘Queen Suzy’ akiwa na babaake.
Mwanadada huyo alijaaliwa kupata mtoto huyo baada ya kuuficha ujauzito wake kwani alikuwa akikaa ndani tu mpaka alipojifungua.
Gazeti hili lilifanikiwa kuzungumza naye ambapo alikiri kujifungua katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na kusema amefurahi sana kupata mtoto wa kike kupitia mpenzi wake wa siku nyingi aitwaye G-Seven.
“Yaani nina furaha ya ajabu kwani ni bahati kwangu ‘kubalansi’, wa kwanza wa kiume, huyu wa kike, namshukuru sana Mungu,” alisema Queen Suzy.
GPL
0 comments:
Post a Comment