2015-02-24

Radi Yaua Mwalimu na Wanafunzi 6 Kigoma.............ina huzunisha sana


Watu saba wakiwamo wanafunzi sita wa darasa la nne katika shule ya msingi Nyakasanda na Mwalimu wa shule hiyo, Anderson Kibada wamekufa baada ya kupigwa na radi huku watu wengine 11 akiwemo Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Laurence Sesegwa (42) wakijeruhiwa.

Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Kigaga Daga alisema kuwa watu hao walifikwa na mauti hayo kufuatia mvua kubwa zilizonyesha zikiambatana na radi zilizoanza majira ya saa tano asubuhi zilizotokea katika kijiji cha Nyachenda wilaya ya Kasulu mkoani.

Mbali na Mwalimu Kibada aliyekufa hapo hapo, Mganga huyo Mkuu wa Wilaya aliwataja wanafunzi kuwa ni pamoja na Mary Steven (11), Severine Mussa (11) na Joseline Joseph (12). 

Aliwataja wanafunzi wengine waliofariki kuwa ni Joyness Simon (14), Nehemia Kepha (14) na Robin Gabriel (14).

Alisema kuwa hadi sasa wanafunzi wanne wanaendelea na matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Kasulu ambao aliwataja kuwa Fadhila Emanuel (13), Matilda Moses (11), Bizimana Manjo (12) huku wanafunzi wengine saba wakiruhusiwa baada ya hali zao kuwa nzuri. 


0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...