2015-02-18

Range Rover ya AY yamdatisha Daz Baba, asema AY ni mfano wa kuigwa na ---------- Yamoyoni


Msanii wa zamani wa kundi la Daz Nundaz, Daz Baba amemmwagia sifa kibao rapper Ambwene Yessayah aka AY kuwa ni msanii wa kuigwa.
AY alitinga kwenye mazishi ya Mzee Ebby Sykes akiwa kwenye Range Rover ya rangi ya kijivu kitu ambacho kilimvutia Daz Baba...


Daz ameiambia Bongo5 kuwa AY ni mshikaji wake toka kipindi cha nyuma na anavutiwa na hustle zake.


AY akiondoka katika makaburi ya Kisutu baada ya mazishi ya Ebby Sykes akiwa kwenye Range Rover

“AY yuko vizuri sana, ni mfano wa kuigwa, mzee wa commercial toka kitambo anafanya muziki mzuri ndo maana unamuona hivyo, ” alisema Daz. “Jamaa anajituma, anafanya kazi kwa bidii ndio maana unaona hayo mafanikio yote,” aliongeza.

Pia Daz amesema kuna mpango wa kufanya ngoma na muimbaji huyo wa ‘Zigo’.

“Nina mpango wa kufanya naye kazi. AY ni mshkaji wangu toka kitambo kwahiyo kila kitu kitaenda sawa.”

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...