Msanii mkongwe katika filamu Bongo, Salome Urassa ‘Thea’.
MSANII mkongwe katika filamu Bongo, Salome Urassa ‘Thea’ amefunguka na kusema kwamba kwa sasa amebadili aina ya maisha yake kwa kuwaepuka marafiki wanafiki aliokuwa akikutana nao kwenye makundi ya majungu.
Akipiga stori mbili tatu na gazeti hili hivi karibuni, Thea alisema siku hizi hata akienda location anafanya kile kilichompeleka na baada ya hapo anarudi nyumbani mapema ili kumuwahi mumewe.
“Siku hizi nikienda location nafanya kilichonipeleka, nabadilisha nguo narudi nyumbani kwangu maana sipendi sana kukaa kwenye vikao yaani makundi maana ndiyo mwanzo wa manenomaneno na majungu hivyo nayaepuka, kwani hayanisaidii pia nimepunguza marafiki maana mimi ni mke wa mtu,” alisema Thea.
GPL
0 comments:
Post a Comment