Muigizaji wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper.
KWAKO muigizaji wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper bila shaka u-mzima wa afya na unaendelea na majukumu yako ya kila siku.Nilisikia siku hizi hutaki tena kuigiza badala yake unatafutiwa biashara ya kufanya, hivi ni kweli? Kwa nini usiendelee na sanaa yako ambayo ndiyo imekufanya uwe maarufu?
KWAKO muigizaji wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper bila shaka u-mzima wa afya na unaendelea na majukumu yako ya kila siku.Nilisikia siku hizi hutaki tena kuigiza badala yake unatafutiwa biashara ya kufanya, hivi ni kweli? Kwa nini usiendelee na sanaa yako ambayo ndiyo imekufanya uwe maarufu?
Ukitaka kujua hali yangu, mimi ni mzima wa afya. Naendelea na mishemishe zangu za kuwahabarisha Watanzania sambamba na kukosoa pale ambapo naona hapako sawa.
Dhumuni la barua hii ni kutaka kukukumbusha kwamba, kwanza wazo lako la kuacha kuigiza sijaliafiki, naomba ulifikirie upya. Umri wako bado unaruhusu kuendelea kufanya sanaa.Kumbuka jina lako limejengwa na sanaa, huna budi kuiheshimu. Bado una deni kubwa la kuifanya sanaa izidi kwenda mbele, ifike hatua na sisi kazi zetu zivuke mipaka.
Ifike hatua filamu zetu ziwe bora na zipendwe kama zinavyopendwa za wasanii wa Nigeria. Kwa nini uache kuigiza? Fikiria upya bwana, utawaudhi mashabiki wako.Ukiachana na suala hilo, suala lingine lililonifanya nimekukumbuka ni baada ya kusikia kuna tetesi kwamba umepangiwa mjengo mwingine unaoishi sasa.
Sikatai wewe ni mtoto wa kike kupewa kitu na mwanaume ni ruksa lakini inabidi uwe makini ili usiwe na maisha ya kumtegemea mtu halafu baadaye akukimbie.Uwe makini ili usiwe mtu tegemezi. Wenyewe mnasema sasa hivi mkiwezeshwa mnaweza, pambana basi ili uweze kusimama mwenyewe.
Kipindi cha nyuma ulipokuwa na mpenzi wako, Dallas, mfanyabiashara maarufu, alikupangishia nyumba ya mamilioni na kukunulia gari la kifahari lakini baadaye mambo yakaenda mrama, ukarudi kwenye nyumba zetu za kawaida.
Hiyo unakumbuka kabisa ilitokana na mwanaume huyo pesa kumpiga chenga, akafikia levo za kina sisi, hakuchi kunakucha na baadaye mkaachana na wewe ukayumba pia.Naamini hiyo ilitosha kuwa funzo kwako, inaonesha umuhimu wa kupambana wewe mwenyewe kuweza kujenga kupitia jasho lako kwani naamini sanaa inalipa hata kama siyo sana.
Niliposikia tena hizi tetesi mpya za wewe kupangiwa mjengo mpya tena wa mamilioni ya fedha, nikasikia na wewe unataka kuacha sanaa, nikaunga kabisa kwamba kuna dalili za wewe kuridhika.
Unajua kuigiza, umbo zuri Mungu kakujalia kwa nini usijikite katika eneo lako la kazi? Anasa zipo lakini kutafuta fedha ni jambo la msingi kwa kila mwanadamu.
Haya mambo ya kutegemea vya watu, watu wenyewe ndiyo hao hawaaminiki ni kujishushia thamani yako mbele ya jamii. Anzisha miradi yako hata kama ni midogo siku moja itakuwa mikubwa na kila mmoja atajivunia mafanikio yako.
Ni matumaini yangu utakuwa umenisoma, nikutakie mafanikio mema katika kazi za mikono yako, tchao!
Wasalaam,
Wasalaam,
GPL
0 comments:
Post a Comment