2015-02-10

ZITTO Z. KABWE, KUWALINDA WATOTO NA MTANDAO?


Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Mh. Zitto Kabwe (Picha ya maktaba)

Dunia inaadhimisha siku ya ya matumizi ya intaneti ambapo kauli mbinu ya mwaka huu ni kubuni kwa pamoja intaneti bora na salama , kwa kuwaajibisha zaidi watumiaji wa intaneti hasa kupitia simu za mkononi. 

Wakati simu za mkononi zenye huduma ya intaneti zikizidi kuongeza kila kukicha, ikiwa matokeo ya maendeleo teknolojia ya kisasa duniani, tishio kubwa kwa sasa ni athari za kimaadili kwa watoto pamoja na vijana wadogo ambao baadhi yao ni miongoni mwa wanaotumia simu za mkononi zenye huduma ya internet-bbc swahili
isome hii:

DUNIA KUSHNEIII: Binti atupia picha kunasa wanaume JIONEE PICHA ZAIDI YA 2 (18+)


Zitto aongoza kwa wafuasi wengi mtandaoni
 

 Utafiti huo uliotolewa hivi karibuni, unaonyesha kuwa mwanasiasa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe anaongoza miongoni mwa Watanzania wanaotumia mitandao hiyo.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, Tanzania ndiyo nchi pekee barani Afrika ambayo mwanasiasa kutoka kambi ya upinzani anaongoza kwa kuwa na wafuasi wengi katika mitandao ya kijamii.

Inaelezwa kuwa hiyo imetokana na ujasiri wake wa kutoa hoja za kashfa za ufisadi pamoja na ubadhirifu katika vikao mbalimbali vya Bunge katika Serikali ya Awamu ya Nne jambo linalomfanya awe mwanasiasa mwenye ushawishi mkubwa zaidi.

Mpaka wakati ripoti hiyo inatolewa, Zitto(38), alikuwa na wafuasi 219,000. Idadi hiyo imeongezeka kwa kiasi baada ya habari hizo kuandikwa na kusambazwa mtandaoni pia.

Kwa rekodi hiyo, Zitto anakuwa ndiye Mtanzania mwenye wafuasi wengi akiwazidi wasanii, wanamichezo na viongozi na wanasiasa wenzake akiwemo Rais Jakaya Kikwete ambaye akaunti yake imefungwa.

Mbunge huyo, mara nyingi hutumia mitandao ya kijamii kufikisha ujumbe kwa wananchi na wafuasi wake popote nchini na duniani kwa ujumla.

Isikupite hii isome: 

Hapatoshi Mbowe: Chadema haitaibiwa kura

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...