2015-03-13

Ahukumiwa Kwenda Jela Miaka 60 na Kuchapwa viboko 12 kwa Kosa la Kubaka Wasichana Wawili Kwa Zamu



Mahakama ya Wilaya ya Bunda, mkoani Mara, juzi imemhukumu mwanamume mmoja Festo Domisian (30), mkazi wa wilayani Ukerewe mkoani Mwanza, kutumikia kifungo cha miaka 60 jela pamoja na kuchapwa viboko 12, baada ya kupatikana na hatia ya kubaka wasichana wawili kwa zamu akiwa na kisu na kumjeruhi mmoja wao.

Hukumu hiyo ilitolewa na Hakimu wa Mahakama hiyo, Hamad Said Kasonso, baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na upande wa mashitaka.

Awali ilidaiwa mahakamani hapo na mwendesha mashitaka wa Polisi Inspekta Hamza Mdogwa, kuwa mshitakiwa huyo alitenda makosa hayo Agosti 14 mwaka jana, majira ya saa 7:00 usiku katika kijiji cha Busambara, kata ya Kibara, wilayani Bunda.

Mdogwa alisema kuwa mshitakiwa huyo aliwaingilia ndani ya nyumba walimokuwa wamelala wasichana hao majina yao yamehifadhiwa kwa sababu ya umri wao kuwa mdogo na kuwatishia kwa silaha aina ya kisu na kuanza kuwabaka kwa zamu.

Alisema kuwa kabla ya kuanza kuwabaka wasichana hao, alivunja mlango wa nyumba yao na kwamba alimjeruhi mmoja wao kwa kumchoma na kisu sehemu ya begani na shingoni na kisha akaanza kumbaka na baada ya kumaliza haja yake akambaka msichana wa pili na kisha akatokomea kusikojulikana.

Aliongeza kuwa kwa vile walalamikaji hao walimtambua kwa sura mshitakiwa huyo walitoa taarifa kwa Ofisa Mtendaji wa kijiji hicho na wananchi wakafanikiwa kumkamata na kumpeleka Polisi.
Akitoa hukumu hiyo Hakimu Kasonso alisema kuwa kosa la kubaka msichana wa kwanza ni kifungo cha miaka 30 jela na kosa la kubaka msichana wa pili pia ni kifungo cha miaka 30, na kwamba adhabu zote zinakwenda kwa pamoja, hivyo atatumikia kifungo cha miaka 30 jela na kuchapwa viboko 12, siku ya kuingia sita na siku ya kumaliza adhabu yake anachapwa vingine sit

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...