2015-03-23

Apewa kilevi kikali anusurika kubakwa ndani ya Gari la Serikali usiku mnene


Duh! Wakati magari ya serikali yanatakiwa kupaki saa 12 jioni, wiki iliyopita mrembo mmoja mkazi wa jijini Dar ambaye jina lake halikupatikana mara moja amefanyiwa kitu mbaya ndani ya gari la serikali usiku mnene baada ya kuzimishwa kwa pombe kali kisha kunusurika kubakwa.

Mrembo huyo akiwa hoi. Tukio hilo lililoshuhudiwa na Ijumaa Wikienda lilijiri mishale ya saa 6:00 usiku kwenye Baa ya Break Point iliyopo maeneo ya Msamvu kandokando ya Barabara ya Morogoro-lringa.

Habari zilizopatikana eneo la tukio zilieleza kwamba dereva wa gari hilo la serikali (namba za usajili zinahifadhiwa kwa sababu maalum) aliyefahamika kwa jina moja la Asenga ndiye aliyedaiwa kuhusika na tukio hilo kwa mrembo huyo aliyetoka naye Dar huku mwenyewe akiwa tilalila.

Baada ya kufotoa picha za tukio huku mrembo huyo akiburuzwa na jamaa hadi kwenye gari kabla ya kupoteza fahamu, mwanahabari wetu alifanya mahojiano na watu mbalimbali ili kupata tukio hilo kwa kina.

Kwa upande wake mhudumu wa baa hiyo aliyekuwa akiwahudumia wawili hao alisema:

”Awali waliagiza bia lakini baadaye mwanaume aliagiza pombe kali yenye thamani ya shilingi elfu 25 na kumlazimisha mrembo huyo kuinywa.

“Jamaa alipoona hivyo alianza kumburuza yule mrembo na kwenda kumlaza kwenye gari lakini watu wakiwemo walinzi walimuona hivyo akashindwa kufanya alichotaka kumfanyia,” alisema mhudumu huyo.



Gari la serikali lililohusika kwenye tukio hilo.

Akihojiwa na mwandishi wetu huku akirekodiwa, dereva huyo alikuwa na haya ya kusema:

”Mimi nimetoka wizarani Dar, nimekuja Moro kikazi.
“Huyu mrembo ni mchepuko wangu nimetoka naye Dar, nilipofika hapa ukumbini nikakutana na demu wangu wa siku nyingi.“Sasa ili niwe na yule wa siku nyingi nikaona nimleweshe huyu akizimika nile raha na yule mwingine.

“Kwanza nimeona umepiga picha kesho nisafishie uniletee,” alisema Asenga akionekana ‘yupo nyingi kichwani’ bila kujua anazungumza na Kamanda wa Oparesheni Fichua Maovu wa (OFM) ya Global Publishers.

Baadaye jamaa huyo aliwaachia walinzi wamlinde mrembo huyo kisha akaendelea na starehe zake kabla ya kutimka na mwanamke huyo kwenye gari.Mathias Daud ambaye ni mlinzi wa baa hiyo alipotakiwa kuzunguzia tukio hilo alisema:“Huyu jamaa anachezea kazi, unajua angemfungia kwenye gari angemuua yule mwanamke.”

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...