Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa akifafanua jambo alipokuwa akifanyiwa mahojiano maalumu na waandishi na wahariri wa magazeti ya Mwananchi Communications Limited, alipotembelea ofisi za magazeti hayo Tabata Relini, Dar es Salaam jana.
Msigwa alisema kwa maoni yake, ni asilimia 20 pekee ya wabunge ndiyo wenye uwezo na vigezo vinavyostahili kupata nafasi hiyo ya uwakilishi wa wananchi katika chombo hicho cha kutunga sheria.
Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa amesema zaidi ya asilimia 80 ya wabunge waliopo bungeni sasa hawakustahili kuwa wabunge kwa sababu baadhi yao wana uwezo mdogo kiakili alioulinganisha na GB moja ya kompyuta.

Mchungaji Msigwa alikuwa akizungumza na wahariri alipotembelea ofisi za Kampuni ya Mwananchi Communications Ltd inayochapisha magazeti ya Mwananchi, The Citizen na Mwanaspoti, Tabata Relini, Dar es Salaam jana.
Alisema wakati umefika kwa Taifa kuweka viwango maalumu vya kuwapata viongozi wa kisiasa wakiwamo wabunge na Rais.
“Tatizo kubwa Watanzania hatuna ‘standards’ (viwango) na vigezo tunavyoviweka kwa mtu anayetaka kuwa kiongozi, yaani tujue kuwa mtu anayekuja kuomba uongozi anapaswa awe mtu wa aina gani.
“Tutakuwa tunafanya makosa makubwa kama Taifa, ikiwa hatutakuwa na ‘standards’. Vinginevyo tutapata hata wasio na sifa ndiyo hawa wanaojitengenezea maandamano kwa kujifanya kuwa ni maarufu.”
Alisema kigezo kinachozingatiwa katika siasa ili kuwa mbunge cha kujua kusoma na kuandika hakitoshi na siyo sahihi, hivyo kinapaswa kitazamwe upya ili kupata wawakilishi watakaoweza kutimiza wajibu wao ipasavyo wakiwa watungaji wa sheria na watetezi wa rasilimali za Taifa.
“Tunaambiwa kigezo muhimu cha kuwa kiongozi akiwamo mbunge ni kujua kusoma na kuandika, hii siyo sahihi kwani kujua kusoma na kuandika pekee hakutoshi kuwa kigezo cha mtu kuwa mbunge au kiongozi,” alisema.
“Kujua kusoma na kuandika siyo kigezo cha kupitia vifungu vya sheria. Unajua kuna baadhi ya wabunge kutokana na upeo mdogo, mtu kama Tundu Lissu akiongea kule ndani (bungeni) hawaelewi, ndiyo maana unakuta wanaishia kumwona kama kichaa.
“Wabunge wengi hawamuelewi Tundu Lissu, kwa sababu vichwa vyao vina ‘GB’ moja za ubongo. Sasa ‘kucontain’ (kukusanya) mambo yote yale ya Bunge, kichwa kinapata moto na ili kupata majibu rahisi, wanasema ni (Lissu) kichaa, maana hawawezi kufikiri kiwango kile kutokana na akili yao kuwa ni ndogo sana,” alisema Msigwa bila kutaja majina ya wabunge hao.
Alisema mbunge anapaswa kuwa na uwezo wa kujieleza, kuelewa mambo, kusoma mambo mengi, akisisitiza kuwa kwa ilivyo sasa ni kama asilimia 20 ya wabunge wote, ndiyo wenye sifa na uwezo wa kujadili mambo.
“Wengi wao wamekaa kaa tu, hawawezi kusema lolote, wabunge wengine tunaposafiri nao, tunashuhudia mambo ya aibu tupu. Wengi wanakuwa kama mabubu, wamekaa kaa tu, hawasemi chochote, hawana michango yoyote, wanasubiri kufanya ‘shopping’ tu kana kwamba wamekwenda kwa ajili hiyo,” alisema Msigwa.
Mwananchi
0 comments:
Post a Comment