2015-03-19

Hili nalo janga!!!!!!!!!! KIGOGO AFUMANIWA AKIVUNJA AMRI YA SITA....tazama picha na video hapa





HILI nalo janga! Mwanaume mmoja anayesemekana ni mfanyabiashara ambaye pia anatajwa kugombea udiwani wa kata moja iliyopo Kinondoni jijini Dar es Salaam, aliyetajwa kwa jina moja la mzee Beno amenaswa akiwa chumba cha gesti na denti wa chuo kimoja kilichopo Kibamba jijini Dar, 



Tukio hilo la aina yake lilijiri Oktoba 20, mwaka huu ndani ya gesti moja (jina tunalo) iliyopo Kimara-Suka jijini Dar es Salaam ambako mama mzazi wa wa binti huyo ndiye aliyemnasa mheshimiwa mtarajiwa huyo na binti yake. 


WASIWASI KWANZA
Awali, mama huyo alisema alianza kuwa na wasiwasi na mwenendo wa binti yake huyo kutokana na kuanza kale katabia ka’ kuchelewa mara kwa mara kurudi nyumbani akitoka chuoni, akajiongeza! 

“Sisi tulishajua binti yetu ameanza katabia kabaya, akienda shuleni anachelewa kurudi wakati si kawaida yake, tukasema kuna jambo linaendelea kwake,” alisema mzazi huyo.

                          Akidhibitiwa baada ya kufumaniwa.
 
USHUSHUSHU
Kwa mujibu wa mzazi huyo aliyeonekana kufura kupita tafsiri ya neno lenyewe, alianza kibarua cha ushushushu kama si upelelezi wa kumfuatilia binti yake ambapo siku moja aliifanyia udukuzi simu yake na kukuta ujumbe mfupi wa maneno (SMS) kwenye simu hiyo ukimtaka afike kwenye gesti hiyo.

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...