Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda ambaye alikuwa amemwandikia Gwajima barua akimwita ofisi kwake, jana mchana alimtembelea hospitalini hapo kwa ajili ya kumjulia hali kiongozi huyo lakini akasisitiza kuwa nia yake bado ipo palepale.
“Nilimtaka leo aripoti ofisini kwangu lakini kwa bahati mbaya anaugua na amelazwa. Nitakwenda kumuona ili nijue hali yake ikoje,” alisema Makonda kabla ya kufunga safari kwenda hospitali alikolazwa.
Alisema pia atataka kiongozi huyo wa kiroho amweleze anavyoelewa maana ya uhuru wa kuabudu unaoelezwa katika Katiba, usajili wa taasisi yake na katiba ya taasisi hiyo.
“Mimi ni mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Kinondoni. Niliagiza polisi wamkamate na baadaye wakimaliza kumhoji aje kwangu pia atahojiwa na jopo la watu 20,” alisema Makonda.
Baada ya kauli hiyo, mijadala kadhaa iliendelea katika mitandao ya kijamii hususani Facebook na Twitter ambapo baadhi ya wananchi walitoa maoni yao wakishangaa na kuhoji uhalali wa DC kutaka kuhoji masuala ambayo yako chini ya mamlaka nyingine kisheria. Yafuatayo ni moja ya maoni hayo yaliyoandikwa kwenye kurasa zao za Facebook.
JULIUS MTATIRO...
YA GWAJIMA vs PENGO
“Polisi wanamuhoji mtuhumiwa ili waone kama ana kosa la kumshitaki au la, hapohapo Mkuu wa Wilaya husika naye anamuandikia barua kumtaka aripoti kuhojiwa na Mkuu wa Wilaya.
"Hakuna Sheria wala Kanuni inayompa mamlaka Mkuu wa Wilaya kujihusisha na upepelezi au ufuatiliaji wa makosa ya jinai. Ni kupoteza muda tu kwa wakuu wa wilaya wanapojaribu kuwaita watuhumiwa wakawahoji, labda pia ni kutojua nini kimewaweka kwenye zile ofisi.
"Pamoja na mimi kutokukubaliana na ujengaji hoja wa matusi uliotumiwa na Mchungaji GWAJIMA kumfikishia ujumbe Kadinali Pengo, namshauri Gwajima asiitikie wito huu wa rafiki yangu, mdogo wangu na kijana mwenzangu DC wa Kinondoni, PAUL MAKONDA, na DC hatakuwa na cha kufanya.
"Wakuu wa wilaya wanahitaji mafunzo zaidi juu ya kazi yao vinginevyo nyadhifa hizi zifutwe tubaki na wakuu wa mikoa na wakurugenzi wa halmashauri. Kwa sababu wakuu wa wilaya wamekosa kazi, sasa wameanza kujishughulisha na upepelezi wa makosa ya jinai. Sina mbavu hapa....”
GODLISTEN J MALISA...
MAKONDA ACHANA NA GWAJIMA, SHUGHULIKA NA YANAYOKUHUSU.!
“Nimecheka sana baada ya kuamka na kukuta Habari kwenye media kuwa eti Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ndg.Paul Makonda amemtaka Askofu Gwajima akaripoti kwake haraka iwezekanavyo mara tu baada ya kutoka Hospitali kwa ajili ya mahojiano.
"Hahahaah hiki ni kituko cha mwaka. Mahojiano gani Makonda anataka kumfanyia Askofu Gwajima? Kwamba Makonda nae amekuwa Afisa Upelelezi wa jeshi la Polisi au?
"Navyoelewa ni kuwa swala la Gwajima ni Criminal Defamation. Ndio maana Jamhuri ikaingilia suala hilo. Na kwa utaratibu wa criminal case ni kuwa Polisi wanafanya upelelezi wao then State Prosecutor anasimama mahakamani dhidi ya mtuhumiwa.
"Sheria zote na machapisho yote ya kisheria yanazohusika na Defamation cases kwa nchi yetu (Defamation Law in Tanzania; Leading Statutes, Cases &Materials) hakuna hata moja inayotoa mandate kwa Mkuu wa Wilaya kufanya upelelezi au kuhoji.
"Sheria ya Kanuni za Adhabu Tanzania (Penal Code) haitoa mandate hiyo. Wala sheria ya Magazeti (Newspapers Act, 1976), wala sheria ya utangazaji (Broadicasting services Act, 1993, wala sheria ya mwenendo wa makosa ya madai (Civil Procedure Code, 1966) wala Sheria ya Ushahidi (The Tanzania Evidence Act, 1966).
"Hizi zote ni sheria zinazodeal na defamation na hakuna hata moja iliyogrant mandate kwa mkuu wa wilaya kuhoji wala kupeleleza. Wala hakuna sheria kati ya hizo nilizozitaja inayosema "Polisi wakishafanya upelelezi Mkuu wa wilaya amuite mlalamikiwa ili ajiridhishe"
"Sasa najiuliza logic ya Makonda kumuita Gwajima kwa mahojiano ni nini? Kwamba anadhani yeye ana nguvu kuliko Polisi? Kwamba anadhani Polisi hawawezi kufanya upelelezi kwa ustadi mkubwa kama yeye? Kwamba haamini upelelezi unaofanywa na jeshi la Polisi?
"Kweli ujinga ni kipaji. Yani kabla hata Polisi hawajamaliza upelezi wao wewe ushakurupuka unataka Gwajima akuone? Akuone ili iweje? Kama ni kuhojiwa ameshahojiwa na Polisi na kama atapatikana na kesi ya kujibu atapelekwa Mahakamani. Sasa wewe unataka akuone ili iweje? Aje akuombee toba au?
"Nadhani Polisi wamzuie huyu "DC wa miezi 6", maana anaweza kuharibu upelelezi unaoendelea kwa kutafuta "cheap popularity".
"Sijawahi kusikia popote duniani, DC anaingilia kesi ambayo upelelezi wake haujakamilika. Hata upelelezi ukikamilika kesi haipelekwi kwa DC inapelekwa mahakamani. Sasa huyu Makonda kapata wapi "kiherehere" cha kumuita Askofu Gwajima.
"Au labda anataka kutubu? Lakini hata kama anataka kutubu angesubiri kwanza Gwajima atoke hospitali, kisha amuite waongee. Sio kuandika mitandaoni na kutangaza kwenye vyombo vya habari eti Gwajima akitoka amuone.
"Gwajima yupo ICU, wewe unatangaza kwenye media eti akitoka akuone.. hii ni akili au matope? Unadhani huko ICU Gwajima anasoma blogu na kusikiliza "Radio Mbao" kama ulivyozitumia kutoa agizo lako? Acha "akili ndogo" kijana.!
"Wakati fulani Mwenyekiti wa CHADEMA Mhe.Freeman Mbowe aliwahi kusema wakuu wa wilaya hawana kazi ndio maana muda mwingi wanatumika kisiasa au kuingilia mambo yasiyowahusu. Mbowe alisema wakuu wa wilaya wana kazi mbili tu kubwa "Kufungisha ndoa na kuandaa vyeti vya vizazi na vifo."
"Hii ya vizazi na vifo kwa sasa inafanywa na RITA, so kwa mujibu wa Mbowe wakuu wa wilaya wamebaki na kazi moja kubwa ambayo ni KUFUNGISHA NDOA .
"Sasa najiuliza hivi Kinondoni hakuna watu wanaofunga tena ndoa zao Bomani ili Mkuu wa wilaya apate kazi za kufanya? Maana Makonda anaonekana hana kazi ndio maana anaanza kuingilia hadi mambo ya kisheria ambayo hayajui kabisa.
"Yani kwenye sheria "this guy is typical tabularasa/layman" Nashauri kama Makonda hana kazi ya kufanya ashughulike na usafi wa mazingira maana manispaa ya Kinondoni bado usafi hauridhishi, asimamie halmashauri izibue mitaro ya maji taka, na kuzuia manyanyaso kwa wafanyabiadhara wadogo.
"Haya masuala ya kisheria aachane nayo maana hayamhusu kabisa na hayawezi.! Wasalaam,”
0 comments:
Post a Comment