Kabuti Onyango si jina geni katika tasnia ya filamu kama upon a mfuatiliaji wa mambo ya Bongo Movies unamjua na unamkubali sana zaidi ya sana kama mpiga picha jongefu bora Bongo bila shaka ana kitu muhimu na cha ziada ambacho ni muhimu sana.
Nakupa siri moja ambayo hauifahamu kuhusu Kabuti, ni mtoto wa mwigizaji mahiri wa filamu na vichekesho Mzee Joseph Onyango ambaye toka ameanza kuigiza hajawahi kupoteza uwezo wake wa kuigiza katika kiwango cha ubora katika tasnia.
Tofauti ya Kabuti na wasanii wengine mara nyingi japo hawezi kuigiza ulazimisha kurithi vipaji vya wazazi wao badala ya kufanya kitu ambacho wanamudu na kuwa mahiri zaidi, kwa Kabuti hilo alilibaini na kugundua kuwa uwezo wake ni kamera na anaikung’uka kweli.
Ana kitu cha ziada mtaalum huyu ana uwezo kuitangaza kazi yake anayoifanya na kuwafikia watu wote kwa wakati, mfano mzuri ni pale msanii huyu alipokuwa akifanya kazi na Salma Jabu ‘Nisha’ sote tulijua sinema ya Nisha iliyokuwa sokoni ijayo na iliyopita.
Baada ya kutengana na msanii huyo Kabuti aliingia makubaliano na mwanadada jembe mtayarishaji makini wa filamu Jennifer Kyaka aka Odama kufungua mlango tu kaingia na kitu cha Jada kila mtu kakubali kuwa Kabuti ni zaidi ya Camerman kwa kifupi jamaa ANAJUA
0 comments:
Post a Comment