Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima.
Imejulikana kwamba kilichomponza Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima (pichani) pamoja na madai ya kutumia maneno yenye kuudhi kwa Askofu wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Polycap Kadinali Pengo mambo ya kisiasa yametajwa kuwa ndiyo msingi wa kushughulikiwa kwake.
Gwajima anadaiwa kushabikia upande mmoja wa kisiasa katika mbio za urais, mwaka huu, huku Kadinali Pengo naye akihusishwa na ufuasi wa upande mwingine.Kikizungumza na Gazeti la Uwazi juzi, chanzo chetu kimoja kilisema kuwa, katika maneno yake ya kumshambulia Kadinali Pengo, Gwajima alisema anaamini Pengo aliyageuka makubaliano ya maaskofu wenzake kwa sababu anamuunga mkono mgombea mmoja wa urais mwaka huu.
Gwajima anadaiwa kushabikia upande mmoja wa kisiasa katika mbio za urais, mwaka huu, huku Kadinali Pengo naye akihusishwa na ufuasi wa upande mwingine.Kikizungumza na Gazeti la Uwazi juzi, chanzo chetu kimoja kilisema kuwa, katika maneno yake ya kumshambulia Kadinali Pengo, Gwajima alisema anaamini Pengo aliyageuka makubaliano ya maaskofu wenzake kwa sababu anamuunga mkono mgombea mmoja wa urais mwaka huu.
“Lakini sasa nawaambia kwamba, hata Gwajima mwenyewe kilichomfanya akazungumza vile ni yeye kuwa upande wa mgombea mmoja wa urais (hamtaji).“Yaani yeye alimsema mwenzake (Pengo) kwamba ametumwa na mgombea mmoja, lakini na yeye pia anatumika kisiasa na mgombea mwingine.
“Ishu ya Gwajima hakuna kingine, ni mnyukano wa kambi za kisiasa (chanzo hakifafanui kambi hizo) na hasa kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu. Maaskofu walikaa wakakubaliana kuwaambia waumini wao wasipigie kura Katiba Inayopendekezwa kwa sababu ya hoja ya Mahakama ya Kadhi, Kadinali Pengo akaja kutoa tamko peke yake kwamba, waumini waachwe waamue wenyewe.
“Pengine Pengo ana mlengo wake ili katiba ipite kwa manufaa fulani, lakini Gwajima naye aliamua kufanya vile kwa sababu anasimamia masilahi ya kundi lake,” kilisema chanzo chetu.Kikaendelea: “Kwa hiyo jamani kama si siasa, Gwajima asingeyasema yale maneno makali vile. Naye alikuwa kazini.”
Gwajima kumnenea maneno yenye kuudhi Kadinali Pengo ndiyo habari ya mjini kwa sasa ambapo, wiki iliyopita, mchungaji huyo alijisalimisha polisi baada ya kutakiwa kufanya hivyo na jeshi hilo.Hata hivyo, wakati Gwajima akihojiwa, ghafla alisikia kizunguzungu na kuanguka ambapo alikimbizwa katika Hospitali Polisi Baracks kisha Hospitali ya TMJ, Dar kwa matibabu zaidi.
Wakati akiendelea na matibabu, inadaiwa juzi usiku wa manane watu 15 walikamatwa kwa madai ya kuonesha mazingira ya kutaka kumtorosha mchungaji huyo.Watu hao walidakwa wakiwa na begi moja la nguo, huku duru za usalama zikidai kuwakuta pia na silaha (bastola) na hati ya kusafiria.
Akizungumza katika mahubiri ya kanisa hilo juzi katika Kanisa la Gwajima lililopo Kawe, Dar, mchungaji mmoja (jina halikupatikana mara moja) alisema kuwa, watu waliokamatwa hawakuwa na lengo baya kwani walikwenda kumpelekea Gwajima nguo za kuvaa. Silaha ilikuwa ndani ya begi, Gwajima anaimiliki kihalali, ingawa hoja inabaki kuwa kwa nini wampelekee nguo za kuvaa usiku wa manane.
0 comments:
Post a Comment