2015-03-18

Mbaroni kutaka kujiunga na Islamic State Bofya Hapa Ujionee Mambo


Wapiganaji wa Islamic State

Mahakama mjini New York Marekani imemfungulia mashitaka mfanyakazi wa zamani wa jeshi la anga kwa madai kuwa alitaka kujiunga na wapiganaji wa kiislam Islamic State.

Waendesha mashitaka wa serikali wanasema kuwa Tairod Nathan Webster Pugh, ambaye alitaka kujiunga na IS wiki moja tu baada ya kufutwa kazi yake ya ufundi wa magari huko nchini Syria.

Hata Pugh mwenye umri wa miaka 47 anatuhumiwa pia kuwa alijaribu kuingia Syria akitokea Uturuki mwezi Januari mwaka huu,lakini alizuiwa na akarejeshwa Misiri baada ya kukataliwa kwenda Marekani.

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...