Na Andrew Chale wa modewji blog
Huenda umesikia mengi juu ya watu wenye uwezo mkubwa wa kiakili na ufahamu hasa wa mambo ama IQ kubwa.
Kwa Tanzania mtoto mwenye IQ kubwa kwa ni Mtoto Nice Valentino mwenye umri wa miaka 3, (Pichani) ameweza kuonesha uwezo mkubwa wa kukariri mambo.
kwa mujibu wa kituo cha Cloud FM cha Tanzania, kimenukuu maelezo kadhaa ikiwemo ya Baba wa mtoto huyo, alieleza kuwa, mtoto huyo alianza kuonesha uwezo tokea akiwa na miezi sita (mtoto mchanga) kwa kufanya vitu vilivyoonesha ishara ya uwezo wa jambo.
Miongoni mwa mambo ambayo yanafanya mtoto Nice kuwa na IQ kubwa ni uwezo wake wa kuongea kiingereza kwa kuhesabu, kusoma na kufanya mambo kadhaa.
“Mtoto wangu ana uwezo wa kuhesabu kuanzia moja hadi 20, wakati hajasoma hata darasa moja. pia anaweza kuhesabu vitu vingi” alieleza baba huyo.
Mtoto huyo Nice Valentino mwenye miaka 3 ametokea wilaya ya Kiteto mkoa wa Manyara. Hajasoma wala kufundishwa na yoyote ila anafahamu hesabu na anaongea Kiingereza tu.
Taarifa hii kwa msaada wa Cloud FM, kupitia kipindi cha Power Breakfast.
0 comments:
Post a Comment