2015-03-18

VIDEO YA MAUNO YAMTESA AMANDA....................ni shiiiiiiiiiiida!!!!!!!!!!!!!


Staa wa filamu za kibongo, Amanda Poshi.  
VIDEO inayomuonyesha msichana anayefanana kwa sura na umbo na staa wa filamu, Amanda Poshi, imemfanya msanii huyo ajikute katika mateso makubwa kisaikolojia, kwani wengi wanaamini ni yeye. 

Akizungumza na gazeti hili, Amanda alisema ameumizwa sana na video hiyo ambapo mwanamke huyo anakata mauno ya haja kwani imesambaa sehemu mbalimbali kiasi cha baadhi ya watu kuwapigia simu wazazi wake wakimlalamikia.

“Jamani mimi siyo huyo mwanamke anayekata mauno na simfahamu, kwanza hata ukiangalia vizuri yeye ni mweusi na siyo mnene kama mimi hivyo nawaomba mashabiki wangu wajue kwamba siwezi kujidhalilisha kiasi hicho,” alisema Amanda.
GPL

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...