Elder Dikam na Kala Nafung wakiwa na nyuso za furaha siku ya harusi yao
Tumezoea kuona vijana au watu wa makamo kufunga ndoa lakini ilikuwa ajabu kwa vikongwe hawa kuchukua uamuzi huo wakiwa na umri mkubwa.
Vikongwe hao Elder Dikam mwenye umri wa miaka 107 na Kala Nafung mwenye miaka 95 kutoka nchini Nigeria wamemua kufunga pingu za maisha huku wakiwashangaza watu kwa uamuzi wao huo kutokanana umri wao.
Imeelezwa kuwa ndoa hiyo ilifungwa kutokana na kila mmoja mwenza wake kufariki dunia na kuwaacha wapekwe hivyo kuamua kutafuta faraja na kukutana kisha kuamua kufunga ndoa
Bibi harusi ana mtoto ana umri wa miaka 65 ambaye ndiye pekee aliyebakia baada ya wengine kufariki.
Ndoa hiyo ilifungwa katika kanisa la Christ in Nations (COCIN) ambapo waliteka watu wengi waliofurika kushuhudia ndoa hiyo huku wakiwapongeza kwa hatua hiyo.
Akisimulia historia ya maisha yake bwana harusi alisema awali alikuwa na wake saba na watoto 32 enzi za ujana wake na wakati huo alikuwa hamtambui Mungu na alikuwa na maisha ya kuoa na kuacha
0 comments:
Post a Comment