Baadhi ya nyumba zikiwa zimezibwa na maji baada ya mafuriko kuikumba wilaya ya Kahama, mkoani Shinyanga
Watu wapatao 50 wamepoteza maisha na wengine kujeruhiwa katika mvua kubwa na mafuriko kaskazini magharibi mwa Tanzania, amesema afisa wa juu.
Mvua kubwa, mvua ya mawe na upepo mkali zimeikumba Wilaya ya Kahama ya Mkoani Shanyanga siku ya Jumanne, na kujeruhi watu wapatao 82.
“Kwa sasa watu wapatao 50 wanahofiwa kupoteza maisha,” Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga aliiambia AFP.
Taarifa zinasema watu wapatao 82 wamejeruhiwa na mafuriko hayo
“Miili mingi ya waathiriwa wanaaminika kubebwa na mafuriko ilikutwa kwenye eneo na wengine waLifariki hospitalini wakati wakipewa matibabu,” alisema wakati akitoa taarifa ya vifo vya watu38.
Taarifa kutoka ofisi ya Rais Jakaya Kikwete ilieleza maafa hayo kama ya, “kushtua na ya kusikitisha”.
Wakazi wa Kahama wakijaribu kusaidiana kuondoka katika eneo hilo baada ya mvua kubwa kunyesha na kusababisha mafuriko yanayohofiwa kuua watu 50
Maafisa walisema watu wanaokadiriwa kuwa 3,500 katika eneo hilo ni wakulima maskini wanaoishi eneo la kusini mwa Ziwa Victoria na karibu na mbuga ya Serengeti, wameathiwa vibaya na mafuriko hayo.
0 comments:
Post a Comment