Msanii wa muziki, Nuh Mziwanda, ametoa kali ya mwaka kwa kudai kwamba kitendo cha kupigwa mara kwa mara na mpenzi wake, Zuwena Mohamed ‘Shilole’, kinampa furaha na ufahamu wa namna anavyopendwa.
Akizungumza na gazeti la Mtanzania, Nuh alisema kupigwa kwake ndo ishara ya mapenzi kutoka kwa mpenzi wake huyo.
“Kwanza kupigwa raha, mpenzi wako asipokupiga hakuonei wivu, mimi nafurahi sana na namtaka anipige tu! kila siku akijisikia, ananidhihirishia kuwa ananipenda,” alisema.
Nuh alisema mengi yamesemwa kutokana na kupigwa kwake mara kwa mara, huku akidai kwamba hilo halina tatizo kwake, kwa kuwa halitaharibu mapenzi yao wanayoamini yatafika mbali.
“Sisi tunawezana na Mungu atusaidie tufikie katika hatua ya ndoa tuliyojiwekea,’’ alimaliza.
0 comments:
Post a Comment