2015-03-09

Sad N eeeeewzzzzz:SHABIKI MWINGINE WA SOKA AJIUA


Deus Ruhinda, raia wa Uganda aliamua kujinyonga baada ya Arsenal kufungwa na Monaco katika mchezo wa Klabu bingwa barani Ulaya.

Mkazi huyo wa katika wilaya ya Mbarara alifikia hatua hiyo baada ya kuwekeana nadhari na mwenzake la thamani ya dola 180. 

Arsenal iliishia kupokea kipigo cha magoli 3-1.

Ruhinda alikua ni dereva wa bodaboda na pesa aliyotumika inasadikiwa kuwa ni ya mmiliki wa bodaboda hiyo anayeishi Kasese. 


Baada ya kushindwa katika bahati nasibu hiyo, Ruhinda aliamua kurudi kijijini kwao ambako alikua hajafika kwa kipindi cha miaka 6. Alijaribu kuwaelezea ndugu zake hali halisi iliyomtokea lakini ndugu walikuwa wakimlaumu kwa nini hakurudi nyumbani kwa kipindi chote hicho. Ndugu hao hawakumpa hata dola moja.

Baadaye Ruhinda alikutwa amejining'iniza kwa kujinyonga katika mti wa mparachichi majira ya mchana siku ya Ijumaa.

Ruhinda aliacha ujumbe wa maandishi ulioelezea kisa cha kujinyonga kwake kuwa ni pesa ya tajiri yake ambayo ameitumia. Ameeleza kuwa bosi wake alimpa pesa hizo ili akamalizie deni la bodaboda anayoendesha na badala yake yeye akachezea bahati nasibu.

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...