Mahakama nchini Brazil imechukua uamuzi wa kufunga huduma za WhatsApp kote nchini na kuwasilisha ombi la kuchunguzwa kwa WhatsApp baada ya kupokea malalamiko na kufunguliwa kwa kesi inayohusu usambazaji wa picha na video za ngono za watoto.
Mahakama iliamua kuchukua uamuzi wa kuzuia matumizi ya WhatsApp kote nchini baada ya kukosa ushirikoano na WhatsApp.
Jaji wa mahakama hakutoa maelezo zaidi kuhusiana na uamuzi huo wala kipindi cha muda ambao marufuku itakapoondolewa.
Kutokana na kupoteza mamilioni ya watumiaji nchini Brazil, WhatsAp inajiandaa kushirikiana na mahakama hiyo.
0 comments:
Post a Comment