KATIKA kile kinachoonekana kama king’ang’anizi, staa wa muziki wa Mduara, Snura Mushi ameibuka na kusema hawezi kuhama nyumba anayoishi hivi sasa, ambayo upande mmoja ni baa kwa vile anaishi kwa malengo na si kufuata watu wanavyosema.
Staa wa muziki wa Mduara, Snura Mushi.
“Kila kukicha nasikia maneno yakizagaa kuwa ninakaa baa hilo litasemwa sana wala sina mpango wa kuhama, nina malengo yangu makubwa, nikihama hapa huenda nikahamia kwenye nyumba yangu na si kwenda kuwatajirisha watu wengine,” alisema Snura.
Alisema kuwa kwake mwanamuziki hakuwezi kumfanya kutafuta kuishi nyumba za mamilioni, kwani siku zote ameishi akitafuta kwa malengo, hivyo hawezi kujikweza kwa kidogo anachopata.
0 comments:
Post a Comment