2015-03-17

Tehama inavyoweza kutumika katika kufundishaji, kujifunza Mambo Mazuri Kama ----------- Utapenda Mwenyewe



Kompyuta ni moja ya nyenzo nzuri za Tehama inayoweza kusaidia mchakato wa ufundishaji na ujifunzaji. Picha ya Maktaba
Na Yona Maro,Mwananchi






Kuanzia mwaka 2011 hadi 2013, nilikuwa mmoja wa wawezeshaji wa mradi wa kuwawezesha walimu wa shule za sekondari kutumia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) katika mchakato wa ufundishaji na ujifunzaji.


Mradi huu ujulikanao kwa jina la Science, Maths and English -ICT Project, ulikuwa unatekelewa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.


Mradi ulilenga masomo ya sayansi, hesabu na lugha ya Kiingereza. Kwa mujibu wa tafiti, masomo haya yalionekana kuwasumbua wanafunzi, hivyo mradi ulikuwa ni mpango wa majaribio wa kutafuta namna bora ya kukabiliana na changamoto hii shuleni.


Walimu walifundishwa namna ambavyo wangeweza kutumia kompyuta pamoja na vifaa vingine kama projekta kwenye ufundishaji.


Lengo kuu lilikuwa ni kutumia Tehama katika kurahisisha ufundishaji wa dhana ngumu ambazo hata pamoja na ufafanuzi wa mwalimu, bado zisingeweza kueleweka kwa wanafunzi.


Kwa mfano, katika somo la Biolojia, mada kama za mifumo ya mmeng’enyo wa chakula, damu na utoaji taka, mwalimu anaweza kutumia vifaa vya Tehama kutazama video au picha zinazoonyesha ufanyaji kazi wa mifumo hiyo.


Zana za Tehama


Katika makala haya, nalenga kumuelekeza mwalimu namna anavyoweza kupata zana za kidijitali za kufundishia na kujifunzia na anavyoweza kuzitumia.


Zana za kidijitali za kufundishia na kujifunzia zinaweza kuwa ni video, tovuti, picha mnato na za kucheza, sauti. Lakini pia unaweza kutumia maandishi yaliyomo kwenye vitabu au kwenye majarida.


Kwa wanaopendelea picha za kucheza, lazima wawe na kompyuta zenye vitumizi kama vile Java na adobe flash player. Vitumizi hivi vinaweza pia kupakuliwa mitandaoni.


Moja ya tovuti nzuri zenye mkusanyiko wa zana za kidijitali za kufundishia na kujifunzia ni PHET. Hadi sasa, tovuti hii ina zaidi ya maelezo milioni 200 ya masomo ya Kemia, Fizikia, Biolojia, Hisabati na mengineyo.


Zana hizi zilizomo kwenye tovuti hii ni za bure. Mwalimu, mwanafunzi au mwingine yeyote hana haja ya kuzinunua, ila unaweza kuchangia kama sehemu ya kuwezesha timu ya waandaaji kufanya kazi yao kwa uzuri zaidi.

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...