Mastaa wa Bongo Movies na watangazaji waliowahi kuwa wapenzi, Bondi Bin Suleiman na Lulu Semagongo ‘Aunty Lulu’ hivi karibuni walipashana baada ya kila mmoja kumdhihaki mwenzake kuwa hana kazi anayofanya mjini.
Bondi alisema kitu kikubwa anachokifanya Aunty Lulu ni kubadilisha wanaume ndiyo sababu ya kushindwa kuendelea na kazi yake ya utangazaji na filamu, akiishia kudanganya kuwa yeye ni mjasiriamali.
Lakini Aunty Lulu naye alijibu tuhuma hizo akisema mwandani wake huyo wa zamani atakuwa anatafuta kitu kutoka kwake, kwani kama ni kazi, hata yeye mwenyewe hana anachokifanya mjini zaidi ya kuuza sura kwani kama anaringia utangazaji, yeye ndiye alimtafutia kazi hiyo.
0 comments:
Post a Comment