Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokea kadi na bendera za aliyekuwa Katibu Mwenezi wa Chadema Wilaya ya Longido ambaye amejiunga na CCM kwenye mkutano uliofanyika
Eworendeke.Ndugu Kinana akiwa ameongozana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wako kwenye ziara ya siku tisa mkoani Arusha ya Kuhimiza,kuimarisha na kutekeleza Ilani ya uchaguzi ya ccm ya mwaka 2010 ikiwemo pia na kusikiliza matatizo ya Wananchi na kuyapatia ufumbuzi.Wananchi wa kijiji cha Eworendeke wakiwa wamekusanyika wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipokuwa akiwahutubia wilayani humo.Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Eworendeke ambapo alitoa salaam za shukrani kwa CCM wilaya ya Longido kwa kuipa ushindi mzuri wakati wa uchaguzi. Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa ujenzi wa nyumba ya watumishi wa Afya katika kijiji cha Lesingeita,wilayani Longido.Pichani shoto ni Mbunge wa jimbo la Longido Mh.Lekule Laizer. Mzee Kitasho Simel Nakutamba akimpa mkono Katibu Mkuu wa CCM ndugu Abdulrahman Kinana mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika hoteli yake ya Longido kama ionekanavyo pichani.Pichani ni jengo la kituo cha mafunzo cha Learning In Longido (LIL),ambapo Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana aliweka jiwe la msingi na kushiriki kupaka rangi kwenye majengo hayo.
0 comments:
Post a Comment