2015-04-08

Askofu wa Kanisa Katoliki Atamani Kumchapa Makofi Waziri


Askofu wa Kanisa Katoliki Mbeya amesema kama angekuwa na Mamlaka dhidi ya Waziri angemchapa makofi Waziri aliyeshindwa kutekeleza kauli ya kuzuia malori yanayoharibu barabara. 

“Yupo Waziri ambaye alisema malori makubwa yanaharibu barabara hivyo mizigo yote inatakiwa kusafirishwa kwa Reli lakini mpaka sasa hajatekeleza.. Kama ningekuwa na uwezo ningemchapa makofi” alisema Askofu Evarist Chengula.


Pamoja na kwamba Askofu huyo hakutaja jina la Waziri huyo lakini aliyekuwa Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe aliwahi kutamka kauli kama hiyo ambapo alipoulizwa kuhusu kilichokwambisha kauli yake amesema kwamba ile haikuwa kauli yake ila ya Serikali, hivyo wa kuulizwa kwa sasa ni Waziri husika wa Wizara hiyo ambaye ni Samuel Sitta.

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...