2015-04-08

Mkazi Wa Kahama Auwa Kwa Kuchomwa Moto Katika Msiba Wa Jirani Baada Ya Kutuhumiwa Kuhusika Na Kifo Cha Marehemu


                    Picha Ya Maktaba

Mkazi mmoja wa Kijiji cha Ulowa Kahama, Chausiku Hamis ameuawa kwa kuchomwa moto na watu waliokusanyika katika msiba wa mtoto wa jirani baada ya kutuhumiwa kuhusika na kifo cha mtoto huyo.

Mtoto huyo mwenye umri wa mwaka mmoja alifariki usiku katika mazingira tata ambapo mwanamke huyo aliuawa baada ya mmoja wa waombolezaji kupandisha mapepo na kumtuhumu Chausiku kuhusika na kifo cha mtoto huyo.

Diwani wa Kata hiyo amesema alipata taarifa za mtoto huyo kuuawa na baadaye kuuawa mwanamke aliyetuhumiwa kuhusika na tukio hilo ambapo Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa na Mtendaji wa Kitongoji hicho walikamatwa na Polisi baada ya nyumba za watu wote kukimbiwa baada ya tukio hilo.

Kamanda wa Polisi Shinyanga, Justus Kamugisha amethibitisha tukio hilo kutokea na kusema kuna watu wawili waliokamatwa kwa ajili ya upelelezi.

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...