MASTAA wana mambo! Baada ya kukataa kwa muda mrefu kwamba hajawahi kuzaa, msanii wa filamu Bongo, Salma Jabu ‘Nisha’ amemwanika mwanaye anayejulikana kwa jina la Iptysam Othman ‘Angel’ mwenye umri wa miaka 10.
Msanii wa filamu Bongo, Salma Jabu ‘Nisha akiwa na mwanae. “Mimi ni mama bora, ndiyo maana nimekuwa nikiulizwa na vyombo mbalimbali vya habari kama nina mtoto nilikuwa nakataa kwa sababu sitaki kumkuza mwanangu kupitia media, ni bora akishakua mwenyewe atajitangaza kupitia kazi zake, sikupenda kumwanika kwenye vyombo vya habari kwa sababu siyo maadili mema,”alisema Nisha.
Salma Jabu ‘Nisha akiwa kwenye pozi. Hata hivyo alikana kwa nguvu zote madai kwamba ana watoto wawili, akisisitiza kuwa anaye mmoja tu na hakutaka kumweka wazi kwa vile aliamini hali ile ingemuathiri kisaikolojia, ingawa hakufafanua.
0 comments:
Post a Comment