2015-01-27

DAAAAAA;VIVA ATAMBA MIMBA YAKE KUWA KAMA YA AUNTY


Musa Mateja/Uwazi
MSANII wa filamu Bongo, Viva ametamba kwamba mimba aliyokuwa nayo ni ya miezi sawa kama ya msanii mwenzake wa filamu, Aunty Ezekiel. 


Msanii wa filamu Bongo, Viva akiwa na Aunt Ezekiel.

Akizungumza na safu hii akiwa katika tamasha moja lililofanyika katika Viwanja vya Leaders, Kinondoni, jijini Dar mwishoni mwa wiki iliyopita, Viva akiwa ameongozana na Aunty huku muda mwingi wakionekana kutambiana mimba zao, alisema huku akimgeukia mwandishi wetu:

“Kwanza nafurahi kuwa na mimba kipindi kimoja na Aunty. Mimba yangu ni kubwa na inazidi hata ya Aunty kwani ina zaidi ya miezi minne sasa, si unaiona.”

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...