HATIMAYE Miss Ruvuma 2008 ambaye pia ni msanii wa muziki wa Bongo Fleva na filamu Bongo, Isabela Mpanda ‘Bela’, ameweka wazi kuwa hataki tena ndoa.
Akizungumza na Uwazi, mwandishi wetu Bela alisema amefikia hatua hiyo baada ya kukaa kwa muda mrefu akisubiri ndoa bila mafanikio na maendeleo yoyote na kuishia kudharaulika katika jamii.
“Sitaki tena ndoa kwa sasa hivi ila ninachohitaji ni kupumzika, hata akitokea mtu siko tayari kwa sasa. Nilishasubiri sana ndoa mpaka hamu imeniisha,” alisema Bela.
0 comments:
Post a Comment