2015-01-29

HAKUNA SIRI TENA;KUMBE NI KWELI JUX ALITOKA NA WOLPER!



Makala: Laurent Samatta

Ukizungumzia kati ya wanamuziki wa R&B Bongo wanaofanya vizuri kwa sasa na usipomtaja Juma Mussa ‘Jux’ utakuwa umekosea sana. 


Msanii wa muziki wa RnB nchini Tanzania, Jux akipozi katika studio za Global TV Online leo.

Jux ni mmoja wa wanamuziki ambao mwishoni mwa wiki iliyopita alitinga ndani ya mjengo wa Global Publishers na kutatua ule utata uliokuwa ukisukuma vichwa vya wengi kuhusiana na kutoka na mwanamuziki mwenzake, Vanesa Mdee ‘Vee Money’.Katika makala haya, Jux anafunguka zaidi kuhusiana na maisha yake kwa ujumla...

Mwandishi: Tayari umeachia video ya Wimbo wa Siskii, kwa nini uliamua kumtumia Vee Money kama ‘video queen’ katika video hiyo?

Jux: Unajua sababu kubwa wakati narekodi huo wimbo, Vanessa alikuwepo pale studio na hadi wimbo unamalizika tayari alikuwa ameshapata wazo la namna video inavyotakiwa kuwa. Nashukuru Mungu ameitendea haki.

Mwandishi: Kuna picha zimetapakaa kwenye mitandao ya kijamii zikiwaonesha wewe na Vanessa kulikoni?

Jux: Mimi na Vanessa tumepiga picha mbili tu, ya kwanza tulipiga ufukweni na ilikuwa baada ya shoo siku ya pili yake. Nyingine ilikuwa kwenye steji na hatukuwa wawili bali wengi.

Mwandishi: Unalizungumziaje suala la wasanii kwenda kushuti video nje ya nchi, hasa Afrika Kusini?

Msanii wa Bongo Movie, Jacqueline Wolper.

Jux: Ninavyoona si sawa kwa sababu watu wa nje kama Wamarekani wanatamani sana kuja kwetu kwa sababu wao kuna vitu hawana.

Jambo jingine ni vifaa, wenzetu wanashuti video kwa kuwa wana kamera za kutosha na wanajua kupiga picha, kuediti na kuchanganya rangi. Kwetu sisi hilo ni tatizo lakini naamini tutafika tu.

Mwandishi: Ni changamoto gani unazokutana nazo hasa ukiangalia wewe ni staa, wanawake hawakusumbui?

Jux:Sisumbuliwi na wanawake, siwezi kusema uongo kama namba zangu za simu zipo za biashara na zipo za binafsi. Kusumbuliwa huwa kunasababishwa na mhusika, mfano nikifanya shoo, nikimaliza huwa naondoka eneo husika hivyo sina nafasi ya wanawake kunisumbua.

Mwanamuziki Vanesa Mdee ‘Vee Money’.

Mwandishi: Kuna wakati tulisikia unatoka na msanii wa Bongo Movie, Jacqueline Wolper ni kweli?

Jux: Hahaha!! Ni kweli kwa sababu sisi ni watu wazima mambo kama hayo yanaweza kutokea. Nilishawahi kutoka naye ila ilikuwa ni muda mrefu sana.

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...