Mchungaji maarufu Afrika Kusini Sthembiso Zondo ambae huwa anatoa mahubiri yake kwa njia ya Redio nchini humo, ratiba ya kurushwa kwa mahubiri yake imesimamishwa kurushwa hewani baada ya kuvuja video inayomuonyesha akizungumza kwenye simu huku akiwa hajavaa nguo yoyote.
Shirika la utangazaji la Afrika Kusini (SABC) limetoa amri ya kusimamishwa kwa Kipindi cha mchungaji huyo hadi itakapotangazwa tena, maamuzi yaliyotolewa baada ya video inayomuonyesha Mchungaji Zondo akiwa hajavaa nguo iliyowekwa kwenye mitandao. Video hiyo inaonyesha kuwa ilirekodiwa na mwanamke aliyekuwa amevaa skirt ya pink lakini hakuweza kutambulika.
Taarifa zinasema kuwa Zondo aliomba radhi kutokana na kuvuja kwa video hiyo, japo kulikuwa na mvutano pia wengine wakilaumu aliyevujisha video hiyo huku wengine wakimfata mchungaji huyo ajieleze kuhusu video hiyo. Bonyeza
0 comments:
Post a Comment