2015-01-19

Mwili wa dereva aliyeuawa kikatili na kunyongwa ndani ya gari umekutwa

 
Mwili wa aliyekuwa dereva wa gari la mizigo Bw Ally Athumani Ally ambaye alikuwa akitafutwa na jeshi la Polisi kufuatia wizi wa milango umekutwa ndani ya gari alilokuwa anaendesha baada ya siku 4 ukiwa umenyongwa na kamba za kubebea mizigo mikubwa huku gari hilo likiwa limeegeshwa kituoni hapo.

Kamanda wa polisi mkoa wa Ilala SACP Mary Nzuki amekili kutokea kwa tukio hilo ambapo baada ya watu hao kufanya mauaji hayo waliuweka mwili huo katika kitanda kilichopo katika gari hilo na kuiba mzigo wa milango uliokuwepo katika gari hilo ambao ulikuwa ukitokea bandarini kwenda katika ghala la mizigo la kampuni ya J Fogh Logistics.

Aidha katika hatua nyingine kamanda Nzuki amesema baadhi ya milango imekwisha patikana na jumla ya watu saba wamekamatwa kuhusiana na tukio hilo ambapo watu hao watafikishwa mahakamani pindi uchunguzi utakapo kamilika.

Akizungumzia tukio hilo dereva mwezake na marehemu Bw Sultani Salum ambaye alifika kituoni hapo kwa ajili ya kuchukua gari hilo amesema kuwa yeye ndiye aliye gundua kuwepo kwa mwili huo baada ya kuona damu ikitokea kitandani na hivyo kulazimika kutoa taarifa ya kuwepo kwa tukio hi

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...