Muimbaji wa Uganda, Jose Chameleone ameuzungumzia uhusiano kati ya Zari Ttale na Diamond Platnumz ambao kwa sasa umekuwa maarufu mno Afrika Mashariki.
Akizungumza na mtandao wa Kenya, Ghafla, Chameleone alisema haoni kama kuna tatizo kwa mastaa hao kuwa wapenzi. “Kama wanapenda, hakuna tatizo,” alisema muimbaji huyo wa Valu Valu.
Akizungumza na mtandao wa Kenya, Ghafla, Chameleone alisema haoni kama kuna tatizo kwa mastaa hao kuwa wapenzi. “Kama wanapenda, hakuna tatizo,” alisema muimbaji huyo wa Valu Valu.
“Diamond hajaoa na Zari pia hajaolewa. Kuwa na uhusiano wa zamani hakumzuii (Zari) kuwa na uhusiano mwingine.”
Kauli hiyo ya Diamond imekuja siku chache tu baada ya Diamond kutangaza kuwa yeye na Zari wanatarajia kupata mtoto wao wa kwanza.
Kwa upande mwingine alipoulizwa kuhusu Diamond kama msanii, Chameleone alisema: Ni msanii mzuri pia.
Namba ya wasanii wazuri Afrika Mashariki inazidi kukua. Ndio maana muziki wetu umeanza kuchezwa Nigeria sababu nguvu ni kubwa kutoka Afrika Mashariki.”
0 comments:
Post a Comment