Makocha na manahodha wengi walichagua mchezaji kwa kuangalia klabu na utaifa
Dar es Salaam. Nahodha wa Yanga na Tanzania, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ ni mmoja wa manahodha watatu kati ya 82 waliopiga kura ya kumchagua Lionel Messi kuwa mwanasoka bora wa mwaka.
Mshambuliaji wa Ureno na Real Madrid, Cristiano Ronaldo amenyakua kwa mara ya tatu tuzo ya Ballon d’Or na kumpiku hasimu wake Messi wa Barcelona na kipa wa Ujerumani, Manuel Neuer akiambulia nafasi ya tatu.
Kila nchi mwanachama wa Fifa utakiwa kupiga kura kwa kuchagua mchezaji bora kati ya watatu waliingia raundi ya mwisho, na Tanzania iliwakilishwa na kocha wa Taifa Stars, Mart Nooij, nahodha Haroub ‘Canavaro’ na Ofisa habari wa Shirikisho soka Tanzania, Boniface Wambura.

Katika kura hizo Tanzania, kocha wa Stars, Nooij alimchagua kwanza Arjen Robben akifuatiwa na Messi na Ronaldo wa tatu, wakati nahodha Canavaro kura yake ya kwanza ilikwenda kwa Messi akifuatiwa na Ronaldo na Neur.
Wakati Msemaji wa TFF, Boniface Wambura naye alienda tofauti na Nooij na Canavaro kwa kumchagua namba moja ni Ronaldo, akifuatiwa na Messi na Neur wa tatu.
Hata hivyo, kocha Nooij si kocha aliyeshangaza watu kupishana katika kura kwani hata Kocha wa England, Roy Hodgson ameshangaza wengi kwa kutompigia kura yeyote kati ya Ronaldo na Messi na badala yake kura yake akaelekeza kwa Muargentina Javier Mascherano kuwa ndio anastahili uchezaji bora wa dunia.
Chaguo lingine la Hodgson lilikuwa kwa Mjeruman Philipp Lahm na kipa Manuel Neuer.
0 comments:
Post a Comment