Nilishangazwa na Bodi ya Ligi kukaa kimya bila kuchukua hatua za haraka kukomesha uhuni huu unaofanywa na baadhi ya timu zikilazimisha ushindi.
Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara, inaendelea katika vituo mbalimbali nchini, lakini mbaya zaidi, ni kutawaliwa kwa vurugu katika ligi hiyo kwa kupigwa waamuzi.
Nilishangazwa na Bodi ya Ligi kukaa kimya bila kuchukua hatua za haraka kukomesha uhuni huu unaofanywa na baadhi ya timu zikilazimisha ushindi.
Vyombo vya habari vinaripoti habari za vurugu hizo karibu katika kila kituo, huku tuhuma za upangaji wa matokeo zikizidi karibu katika kila kituo, lakini hakuna hatua za haraka kukabiliana na hali hii.

Nilisikia habari moja ambayo pengine inawezekana kunishawishi, kwa nini Shirikisho la Soka Tanzania (TFF ) na Bodi yake ya Ligi ziko kimya, kwamba kuna baadhi ya timu zinapigiwa chapuo kupanda Ligi Kuu.
Ni kwa utashi wao au utashi wa kisiasa, baadhi ya timu zinatakiwa, piga ua, lazima zipande, sijui kama kuna ukweli wa hili, lakini wahenga walisema lisemwalo lipo.
Kwa bahati nzuri, hata viongozi wa klabu hizo zinazopigapiga, wamekuwa wakiripotiwa kwenye vyombo vya habari wakilalamikia kuonewa kwenye viwanja vya ugenini na baadaye wao kutoa ahadi kuwa timu zitakazokwenda kwenye vituo vyao zitashughulikiwa kama zilivyoshughulikia timu nyingine.
Kila siku na inaonekana, timu za majeshi ndizo zinaongoza kwa kufanya fujo ndani na nje ya uwanja, huku zikitumia kauli kwamba Ligi Daraja la Kwanza haina mwenyewe na hivyo zinafanya mambo zinavyotaka.
Haiwezekani uhuni huu kufumbiwa macho. Sumu ya saratani huenea taratibu na mwisho wa siku, timu zinazopanda, zitaendeleza sumu hiyo.
Baada ya kukithiri kwa matukio ya vurugu, nilisikia Bodi ya Ligi inataraji kutoa adhabu kali kwa Polisi Dodoma, Villa Squad na Friends Ranger.
Ofisa wa Bodi ya Ligi, Joel Balisidya alikaririwa akisema kuwa bodi haiwezi kuvumilia vitendo vyovyote vya uvunjifu wa amani michezoni.
Nakubaliana na ndugu yangu Balisidya, Ofisa wa Bodi kwa hili la kukaa na kupitia ripoti za matukio yote na kutoa adhabu kali kwa mujibu wa sheria zinazoendesha Ligi Daraja la Kwanza ili iwe fundisho kwa wengine.
Timu hizi siyo za kuendekezwa. Kila aliyekuwa uwanjani ameona vurugu, kila aliyeguswa alisikitika kwa kadri nafsi yake ilivyohisi, sasa hakuna sababu ya kuziachia. Bodi ya Ligi izifute tu Ligi Daraja la Kwanza, zikajipange upya kinidhamu, lakini siyo kupewa onyo kali.
0 comments:
Post a Comment