MSANII wa muziki wa Hip Hop, Emmanuel Simwinga ‘Izo Business’, amesema licha ya kushauriwa na rafiki zake kuingia kwenye siasa, bado hajaona umuhimu wa kufanya hivyo.
Akizungumza na MTANZANIA jana, Izo Business alisema hakuna umuhimu wa kuingia kwenye siasa, kwani inatakiwa mtu ajitoe kwa ajili ya watu na siyo kuingia ili ujipatie fedha kama yalivyo mawazo ya wasanii wengi.
“Siasa kwa upande wangu sijaipa kipaumbele, ingawa nimeshawishiwa na marafiki zangu nigombee nafasi mbalimbali,” alisema Izo Business.
Alisema wale waliojihusisha na siasa wasisahau kuwatumikia wananchi waliowapa nafasi hizo, kwani wengi wamekuwa wakijisahau na kuishia kufuja fedha za Serikali.
0 comments:
Post a Comment