Mwigizaji mkongwe wa vichekesho hapa Bongo, Rashid Mwinshehe "Kingwendu", amesema anajiandaa Kugombea Ubunge 2015 Kupitia Chama ambacho amedai Kuwa anaona Kinapendwa na Watanzania wengi bila ya Kutaja Jina la Chama hicho wala Jimbo atakalogombea.
Wataalamu wa Masuala ya Kisiasa Nchini, wameitafsiri Kauli hiyo ya Kingwendu Kwa Mitazamo tofauti, huku Wengi Kati yao Wakisema Kuwa Upinzani Una Nguvu Kubwa hivi sasa hapa Nchini, hivyo Sio ajabu Kwamba yawezekana Msanii huyu amevutiwa na Kuamua Kujiunga na Chama fulani Cha Upinzani Ili aendeshe harakati za Ukombozi wa Taifa hili.
Akizungumza na Mwandishi wa Tanzania Daima, Kingwendu alisema, "Ninajiandaa Kugombea Ubunge 2015 Kupitia Chama ninachoona Kinapendwa na Watanzania wengi Kwenye Jimbo ambalo ntalitaja hapo baadae Wakati Utakapofika...
"Bado ninafanya Mazungumzo na Washauri wangu wa Karibu Kuhusiana na Swala, nadhani ntaliweka Wazi muda Ukifika..."
0 comments:
Post a Comment