Mwanasoka bora wa FIFA 2014 Cristiano Ronaldo hatimaye jana usiku amepata bao lake la Kwanza baada ya ukame katika takriban michezo mitatu aliyocheza tangu amalize kutumikia adhabu yake.
Ronaldo amefunga bao la Kwanza dakika ya 26 akiiongoza Real Madrid kupata ushindi wa mabao 2-0 nchini Ujerumani dhidi ya Schalke 04 katika mchezo wa kwanza wa 16 bora wa Mabingwa Ulaya.
Bao la Pili limefungwa na Marcelo katika dakika ya 79 na kuiweka Real Madrid katika nafasi nzuri ya kufuzu Robo Fainali kwa kuwa katika mchezo wa marudiano utakaopigwa Machi 10 nchini Hispania, Real Madrid itahitaji sare yoyote ili kusonga mbele.
Katika mchezo mwingine FC Basel imetoshana nguvu kwa kutoka sare ya bao 1-1 na FC Porto mchezo uliopigwa nchini Uswisi.
Bao la Basel limefungwa na Derlis Gonzalez dakika ya 11, huku Danilo akiisawazishia Porto kwa mkwaju wa penati dakika ya 79.
Mechi za marudiano kwa michezo ya leo zitapigwa Machi 10, 2015
0 comments:
Post a Comment