ONESHO la burudani ya warembo lililoitwa Miss Valentine, lililofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita katika Ukumbi wa Vybe mjini hapa kusherehekea siku hiyo ya wapendanao, liligeuka kuwa kichefuchefu mbele ya aliyekuwa mgeni rasmi, Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Didas Masaburi.
Mrembo akipita jukwaani katika onesho la burudani ya warembo lililoitwa Miss Valentine huko Morogoro.
Mmoja wa warembo walioshiriki onesho hilo, ambaye jina lake halikupatikana mara moja, alipita jukwaani akiwa amevalia nusu utupu, hali iliyosababisha mamia ya mashabiki waliofurika ukumbini hapo kumzomea kwa sauti kubwa.
Zomeazomea hiyo ilimshtua mwandaaji wa onesho hilo, Alex Nikitasi ambaye alipanda jukwaani na kumkinga msichana huyo asipigwe picha na mwandishi wa gazeti hili, kabla ya kumtolea maneno ya dhihaka.
Nikitasi ambaye pia ni mwandaaji wa Shindano la Redds Miss Kanda ya Mashariki kwa zaidi ya miaka mitano, alisikika akisema; We Shekidele unataka kumtoa mrembo wangu kwenye magazeti yako ya udaku, sitaki umpige picha.
Mrembo mwingine akitembea jukwaani katika onesho hilo.
Baadhi ya watu waliohudhuria onesho hilo walilaani kitendo cha mrembo huyo kupita na vazi hilo na mwandaaji wake kumtetea, wakisema vitendo kama hivyo vinashamiri kwa sababu wanaopaswa kuvidhibiti, wanavitetea.
Ingawa hakusema lolote, lakini Mstahiki Meya na wageni wengine wa jukwaa kuu hawakuonesha kufurahishwa na kitendo hicho cha kukiukwa kwa maadili waziwazi.
0 comments:
Post a Comment