Siku zote unapopita kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa kuna ukaguzi mkubwa ambao kila abiria huwa anafanyiwa kabla ya kuingia kwenye ndege ambapo hulazimika kuvua saa yako, kuziweka simu pembeni na vitu vingine ikiwemo kuvua viatu na mkanda kabla ya kupita kwenye mashine maalum ya ukaguzi.
Hii imetoka Russia kwenye uwanja wa ndege wa Pulkovo ambapo abiria mmoja aliekerwa na ishu ya Askari kusachisachi kwenye mashine maalum yenye mfano wa mlango, aliamua kuvua nguo zote baada ya kukasirishwa na hilo zoezi.
Maamuzi ya kuvua hizo nguo ni ili kuwapa askari urahisi wa kufanya ukaguzi ambapo aliwaacha hoi Wafanyakazi wa uwanja wa ndege na abiria wengine pia huku Polisi wakiwa kimya bila kuzungumza chochote akapita zake.
Angalia video hapa chini au bonyeza
0 comments:
Post a Comment