2015-02-03

Maswali kumi kwa mbunge wangu Aliko Kibona

 
                                              Aliko Kibona

Uliahidi wakulima wote wa Ileje watapata mbolea ya ruzuku, lakini sasa haipatikani, nini kimekwamisha mbolea ya ruzuku mwaka huu?

1. Daniel Mlwafu, mkazi wa Itumba.

Wewe na Rais Jakaya Kikwete wakati wa kampeni za 2010 mliahidi kujenga barabara ya lami kutoka Mpemba hadi Isongole, lakini hivi sasa hakuna dalili wala maelezo kwa nini jambo hilo halijatekelezwa.

Jibu: Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi imekamilisha hatua zote zinazotakiwa hadi kuanza ujenzi wa barabara. Kwa sasa kazi hiyo kama vile upembuzi yakinifu imekamilika na hatua iliyobaki ni kutafuta fedha. 


2. Farida Swila, mkazi Isongole.

Kwa nini hutusaidii kutafuta wanunuzi wa mahindi ya mwaka jana ambayo hadi sasa yamejaa kwenye nyumba zetu baada ya kukosa soko?

Jibu: Juhudi za Serikali kutafuta soko la mahindi zimefanyika na mimi nimeitaarifu Serikali kuwa Ileje kuna mahindi ya kutosha hivyo kupitia Wakala wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) wamefika na kununua. Malipo yatafanyika ndani ya mwezi wa pili. 


3. Calorine Nakabuja, mkazi wa Itumba.

Ulituahidi kutusaidia mikopo wanawake kupitia Saccos, lakini mpaka sasa muda wako unamalizika hujatusaidia, kwa nini ulitudanganya?

Jibu: Mikopo ya wanawake na vijana inategemea makusanyo ya ndani ya halmashauri. Tunategemea baada ya kupata ushuru wetu kutokana na mahindi yaliyonunuliwa tutawapatia kina mama na vijana mikopo. Binafsi nimetoa fedha wa ajili ya Vicoba, Itale, Ilondo, Sheyo, Itega, Igoje na Ndola.


Mwananchi.

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...