Picha mbalimbali zikimuonyesha Diamond na Zari kwenye viunga vya Forodhani visiwani Zanzibar.
Katika kile kinachoelezewa na wengi kupitia mitandao ya kijamii na baadhi ya watu walioongea na mtandao huu wa modewjiblog, wamefunguka juu ya kitendo cha mwanamuziki nguli Nchini, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ kutinga visiwani Zanzibar akiwa na wapambe wake pamoja na Boss Lady Zari ‘asali wa moyo wake’ ni mbwe mbwe za kumzima Ali Kiba ambaye alitikisa vilivyo katika shoo yake kwenye tamasha la Sauti za Busara 2015.
Wadadisi wa mambo ukiwemo mtandao huu wa modewjiblog ambao ulikuwa visiwani humo katika tamasha hilo la 12, la Sauti za Busara 2015, mji mzima wa Zanzibar kila kona ilikuwa ni habari ya Ali Kiba, ambaye aliweza kutikisa jukwaa la Sauti za Busara vilivyo ikiwemo kuimba nyimbo zaidi ya 12, akiimba ‘live’ bila kutumia ‘CD’ ama ‘play back’ kama wafanyavyo wasanii wengi hasa wa Tanzania.
Ali Kiba alipiga shoo hiyo Februari 12, kwenye siku ya kwanza ya tamasha hilo kubwa la saba kwa Bara la Afrika, linalokuza muziki duniani kote.
Kwa kile kilichoelezewa kuwa alifika kuzima mbwe mbwe za Ali Kiba, ni pale Diamond na Zari walipotimba viunga vya Forodhani na kisha kuanza kufanya utalii wa ndani kwa kuangalia vyakula mbalimbali vikiwemo vya baharini ‘sea food’, vyakula vya asili vya kisiwa hicho na vyakula vingine, ambapo watu walipowashtukia kuwa ni Diamond na Zari, umati wa watu wakawa wanawafuata nyuma huku wakitaka kupiga naye picha.
Hatua hiyo ilifanyaa eneo hilo la Forodhani kuwa dogo kwani ghafla mastaa hao wakaanza kuwekewa ulinzi na wapambe wao ili watimize kile wanachotaka na kilichowaleta hapo.
“Kama unavyowajua Wazanzibar walivyo ‘ngangari’ licha ya kuzuiwa kumsogelea Diamond, lakini waliweza kufanya kile kinachoitwa ‘Ngunguri’ na kupenya hadi kupiga naye picha kitendo kilichomfanya Diamond kukubali matokeo.
Tukio hilo lililodumu kwa muda wa zaidi ya dakika 15, mpaka Diamond na wapambe wake wanapotea kwenye viunga hivyo, Watu mbali mbali hususani wanawake walikuwa wakifurika kwa wingi kwa lengo la kumuona na hata kupiga naye picha.
Tukio hilo lililodumu kwa muda wa zaidi ya dakika 15, mpaka Diamond na wapambe wake wanapotea kwenye viunga hivyo, Watu mbali mbali hususani wanawake walikuwa wakifurika kwa wingi kwa lengo la kumuona na hata kupiga naye picha.
Ali Kiba akitoa burudani tamasha la Sauti za Busara 2015.
Hata hivyo, baadhi ya watu waliomkosa pamoja na baadhi ya waliomshuhudia eneo hilo la Bustani, walibainisha kuwa, Diamond alikuja kuzima upepo wa Ali Kiba.
“Ali Kiba, katikisa sana Sauti za Busara kwenye shoo yake hakuna anayemfikia, ujio wa Diamond amekuja kupima upepo tu si bure” alisema Bayu, mmoja wa wadau wakubwa wa muziki wa kizazi kipya, Bongo fleva.
Mbali na Bayuu, wengine walianza kuibua mijadala ya hapa na pale wakihoji ujio wa Diamond kwani kwa sasa wamekuwa na ‘bifu’ na Ali Kiba licha ya wote kukanusha kwa nyakati tofauti huku kubwa likiwa nani mkali zaidi.
Kwani bifu lao hilo pia lilipelekea kila wawili hao wanapopiga shoo ya pamoja, mmoja wapo kuzomewa ama kutupiwa mawe, hali iliyomkutana Diamond zaidi ya mara mbili katika shoo tofauti ambazo walikutanishwa steji moja kwa kile kinachoelezwa kuibuka kwa makundi ‘#Teamkiba’ na #TeamDiamond’.
Umati wa wadau kutoka kila kona ya dunia waliohudhuria tamasha la Sauti za Busara 2015.
Hata hivyo, siku hiyo hiyo ya Diamond ambayo alikanyaga visiwani hapo, pia Ali Kiba alikuwa na shoo nyingine binafsi ya siku ya wapendanao, ambapo ilisemekana wapambe wa Diamond walienda kupima ‘upepo’ wa jamaa huyo Ali Kiba.
Hivyo, kama ilivyo kawaida yake, Diamond, aliweza tupia picha mbalimbali ya matukio yaliyotokea visiwani humo, huku kikubwa akiwa na Boss Lady Zari wakitanua raha. Diamond alimwelezea Zari kuwa ndio mara yake ya kwanza kukanyaga visiwani humo hivyo kwa kiasi kikubwa ‘alikuwa mshamba’ kwani mtandao huu ulishuhudia boss lady huyo akiangalia kila chakula kwenye viunga vya Forodhani huku baadhi ya vyakula akionesha kuviogopa.
Katika hatua nyingine, Mastaa mbalimbali kwa muda wa wiki moja waliweza kuiteka Zanzibar ikiwemo kwenye tamasha la Sauti za Busara. Mastaa hao wakiwemo wanamichezo, wanamuziki, wasanii, modoz, designers kwa pamoja walikuwa wakirandaranda kwenye viunga vya Zanzibar.
Diamond na Boss Lady Zari wakiwa katika pozi za kimahaba kwenye hoteli waliyofikia visiwani humo.
Miongoni mwa mastaa hao ni Martin Kadinda ambaye hata hivyo uwepo wake Visiwani Unguja ulizua na kuezua maswali mengi, kwani licha ya kuonekana pekee yake, ilidaiwa kuwa alikuwa na Wema Sepetu, ambaye alibaki hoteli.
Mastaa wengine ni msanii wa hip hop, Farid Kubanda ‘Fid Q’, star wa tamthilia ya Siri ya Mtungi, Juma Rajab ‘Cheche’ ama Zoba na wengine.
Mahaba niuwe….!
Bata likiendelea kwenye fukwa za visiwani Zanzibar.
0 comments:
Post a Comment