2015-02-25

UEFA: Matokeo ya Michezo ya Jana Man City vs FC Barcelona, Juventus Vs Borrusia Dortmund yako hapa

Mshambuliaji aliyejiunga na Barcelona akitokea Liverpool msimu uliopita Luis Suarez amekumbushia cheche zake nchini England kwa kuiongoza timu yake ya sasa ya Barcelona kuikaanga Manchester City kwa kuichapa 
mabao 2-1 Katika mchezo wa hatua ya 16 bora ya Kombe la Mabingwa barani Ulaya. 

Katika mchezo huu uliopigwa Etihad Stadium, Barcelona wameanza kujipatia mabao yao katika dakika ya 16 na 30 kupitia kwa Luis Suarez ‘Mnyama’ na wenyeji 
\Manchester City wamepata bao lao kupitia kwa Sergio Aguero dakika ya 69 huku Gael Clichy akitolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 74 baada ya kupata kadi ya njano ya pili.

Katika dakika za majeruhi, Lionel Messi amekosa penati iliyochezwa kwa ustadi na kipa wa City Joe Hart, penati iliyopatikana baada ya Zabaleta kumchezea vibaya Messi katika eneo la hatari 

Timu hizi zitarudiana Machi 18, 2015 katika dimba la Camp Nou nchini Hispania. 

Timu hizi pia zilikutana katika msimu uliopita katika hatua kama hii na Barcelona kuitupa nje Manchester City kwa jumla ya mabao 4-1.
Je, uonavyo wewe historia hii itajirudia? 

Mechi nyingine imepigwa Juventus Stadium Turin nchini Italia kati ya Juventus na Borrusia Dortmund na kushuhudia Juventus ikiichapa Borussia Dortmund mabao 2-1. 

Marudio ya mechi hii pia ni Machi 18 katika dimba la BVB Stadion Dortmund nchini Ujeruman

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...