2015-02-18

Yanga, Azam pongezi kuwadunda El-Merreikh, BDF XI


Chama cha kandanda mkoa wa Dar es salaam DRFA,kimewapongeza wawakilishi wa Tanzania bara katika michuano ya vilabu barani Afrika klabu ya Azam FC na Yanga SC,kwa kuanza na ushindi katika mechi zao za mkondo wa kwanza mwishoni mwa juma.

Yanga walikuwa wa kwanza kuwapa raha Watanzania siku ya Jumamosi katika uwanjwa wa Taifa jijini Dar es Salaam,baada ya kuifunga mabao 2-0 timu ya maafande wa Polisi toka Botswana, BDF 11,mabao yete hayo yakitupiwa nyavuni na mshambuliaji Amis Tambwe,ikiwa ni mchezo wa kuwania kombe la Shirikisho (CAF Confederation Cup).

Kwa upande wa Azam FC,wao waliwafunga wababe wa soka huko Sudan klabu ya El-Merekh kwa mabao 2-0 yaliyofungwa na Didier Kavumbagu pamoja na John Rafael Bocco,katika mchezo wa kuwania kombe la klabu bingwa uliopigwa katika dimba la Azam Complex Chamazi.

Mwenyekiti wa DRFA,Almas Kasongo,amewapongeza wawakilishi hao wa Tanzania kwa hatua hiyo nzuri waliyoanza nayo,na kusema kuwa maandalizi yaliyofanywa na vilabu hivyo kuelekea mashindano hayo ya Afrika,pamoja na ubora wa wachezaji na makocha,ni dhahiri kwamba vitafanikiwa kuvuka katika hatua hiyo ya kwanza.

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...