2015-03-10

Kamati ya Zitto yataka ATCL mpya kuundwa


Kauli hiyo ilitolewa kwenye ofisi ndogo za Bunge Dar es Salaam wakati wa kikao cha mashauriano baina ya TR, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na Kamati hiyo kilichofanyika jana na kukubaliana kuwa TR asimamie mchakato huo.

Dar es Salaam. Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC), imetoa siku 113 kwa Msajili wa Hazina (TR), Lawrence Mafuru kukamilisha mpango mkakati wa kuanzisha upya Shirika la Ndege Tanzania kwa kushirikiana na Mamlaka za Hifadhi za Ngorongoro na Tanapa.

Kauli hiyo ilitolewa kwenye ofisi ndogo za Bunge Dar es Salaam wakati wa kikao cha mashauriano baina ya TR, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na Kamati hiyo kilichofanyika jana na kukubaliana kuwa TR asimamie mchakato huo. 

Mwenyekiti wa PAC, Zitto Kabwe alisema: “Baada ya majadiliano kamati inamuagiza TR asimamie mchakato huu ambao umekwisha anza miaka miwili iliyopita kuhakikisha ifikapo Juni 30, iwe imewasilisha ripoti yake kabla ya Bajeti ya Serikali kuleta mpango mkakati huo.”

Zitto aliongeza kuwa, “Tunataka kuwa na shirika jipya linaloweza kujiongoza na TR ndiye ana wajibu wa hilo, mchakato huu ulipoanza haukuwa umesimamiwa vizuri kwani hata TR mwenyewe hakuwa anaufahamu lakini sasa tunamkabidhi jukumu hilo yeye mwenyewe.”

Alisema mapato wanayopata Tanapa na Ngorongoro yanaweza kununua ndege na wala si kuchangia mapato kama ilivyokuwa awali. 


Kwa upande wake, Mafuru alisema: “Mimi nitakwenda kutumia taarifa za kamati ambazo zilikwisha undwa na kuangalia jinsi gani shirika litafufuliwa pamoja na maoni ya kamati kisha nitakuja na kile ambacho kamati imekipendekeza.”

Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), Salim Msoma alisema, suala la wawekezaji hususani wa nje halitakiwi kutegemewa kwani linapokuja katika utekelezaji wake, miradi yake inakuwa na changamoto nyingi.

Mwananchi

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...