2015-03-05

KIKWETE KUZINDUA STUDIO ZA AZAM TV KESHO


Naibu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam Media Group Tido Muhando akiongea mbele ya waandishi wa habari juu ya uzinduzi wa kituo hicho hapo kesho.

Mkurugenzi uendeshaji wa vipindi vya Azam TV, Yahaya Mohamed, akifafanua jinsi vipindi vyao vitakavyoboleshwa.Mtangazaji wa Chanel Ten Saidi Makala akiuliza swali juu ya uzinduzi huo utakavyokuwa.

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais Jakaya Mrisho Kikwete, mapema kesho anatarajia kuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa studio na ofisi kwa ujumla za Azam TV.

Akizungumza mbele ya waandishi wa habari Naibu Afisa Mtendaji Mkuu wa Azam Media Group, Tido Muhando alisema kwamba, uzinduzi wa studio na ofisi mpya za kituo hicho utafanyika kesho saa 4 asubuhi huku mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete.

“Kesho tunatarajia kuzindua ofisi zetu mpya hapa Tabata Relini, ambapo Rais wetu Jakaya Kikwete ndiyo atatuzindulia kuanzia majira ya saa 4 asubuhi, tunatarajia mara baada tu ya mheshimiwa rais kukamilisha uzinduzi huo, tayari tutaanza kuonyesha program zetu mpya, na mambo yote ya kiofisi yataanza rasmi,”

“ Kiukweli kabisa napenda tu kuwafahamisha wapenzi wote wa Azm TV kuwa kituo chetu kitakachozinduliwa kesho, kitakuwa cha kwanza kwa ubora hapa Afrika mashariki na kati, maana tumetumia zaidi ya Dolla milioni 31 kwaajiri ya kukiandaa, hivyo huduma na watangazaji wetu tunatarajia watakuwa na hadhi na ubora unaoendana na kituo chetu maana ni kikubwa na kina hadhi ya kimataifa zaidi,” alisema Tido Muhando.

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...