2015-03-18

Kinana: UKAWA Utabadilika na Kuwa UKIWA Ifikapo Oktoba



Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana ameubeza muungano wa vyama vya upinzani, maarufu kama Ukawa na kusema muungano huo utabadilika jina ifikapo mwezi Oktoba mwaka huu na kuitwa Ukiwa, baada ya Chama Cha Mapinduzi kutangazwa kuwa mshindi katika nafasi ya Urais.

Kinana alisema mabadiliko hayo ya jina, yanatokana na kelele nyingi pamoja na mikakati mingi wanayoizungumza ya kuchukua madaraka ya Urais, jambo ambalo alilisema ni sawa na ndoto ya Abunuasi.

Alisema siku zote mtu yeyote au chama chochote kilicho na mikakati, hakielezi mikakati yake hadharani, kama wanavyofanya viongozi hao wa Ukawa katika majukwaa mbalimbali wanayozungumza.

Alisema mbali na hayo, vyama hivyo vya upinzani bado havijaaminiwa vya kutosha na wananchi katika kuongoza nchi, hali ambayo bado inawapa wakati mgumu zaidi kwa kuwa watanzania wengi wameendelea kukiamini chama cha mapinduzi.

Alisema pamoja na mikakati hiyo wanayoieleza, ukiwemo wa kusimamisha mgombea mmoja wa nafasi ya Urais, bado mpango huo unakabiliwa na changamoto nyingi, ikiwemo ya kila chama kutaka kuwa na mgombea wake katika nafasi hiyo.

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...